TREY SONGZ MATATANI TENA

0
813

PHILADELPHIA, MAREKANI

NYOTA wa muziki nchini Marekani, Trey Songz, ameingia matatani tena kwa mara ya pili baada ya kumshambulia shabiki wake wa kike katika kumbi ya starehe ya Vanity Grand Cabaret.

Kwa mujibu wa TMZ, mrembo huyo aliamua kwenda kwenye kumbi hiyo kwa ajili ya kumwona msanii huyo ambaye amekuwa shabiki wake kwa kipindi kirefu na kutaka kupiga naye picha, lakini Trey Songz aliamua kuichukua simu ya mrembo huyo na kumpiga nayo usoni.

Kutokana na kitendo hicho, Trey Songz, amefikishwa mahakamani na kutakiwa kulipa dola 50,000 ambazo ni sawa na 111,288,000 za Kitanzania.

Miezi minne iliyopita msanii huyo alikuwa na kesi mahakamani kwa tuhuma ya kumshambulia polisi Desemba mwaka jana.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here