27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

TRENI YA ABIRIA YAANGUKA PWANI

Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM


TRENI ya abiria ya Deluxe iliyokuwa safarini kutoka Kigoma kuelekea Dar es Salaam, imepata ajali katika Stesheni za Ngeta na Ruvu mkoani Pwani.

Ajali hiyo ilitokea jana jioni baada ya kuacha njia na kusababisha mabehewa kuanguka.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Midladjy Maez, alisema ajali hiyo ilihusisha mabehewa matano na  kati ya hayo manne yalikuwa ya abiria na moja ni lile la breki linalokaa nyuma.

Alisema  mabehewa mawili yaliacha njia na matatu yalianguka.

“Hiyo treni ilikuwa inatokea mkoani Kigoma na ilitakiwa kufika Dar es Salaam saa 11:30 jioni, lakini muda huu (saa 10:39 jioni) tumepata taarifa kwamba imepata ajali, bado tunaendelea kufuatilia kujua kama kuna majeruhi,” alisema Maez.

Alisema tayari wahandisi na mafundi wa TRL wameelekea katika eneo ilikotokea ajali hiyo.

Alisema ilitokea saa 9:40 alasiri ambapo wapo kadhaa wamejeruhiwa na mmoja hali ni mbaya.

“Kikosi cha uokoaji kikimaliza kazi ya kuinua mabehewa ndipo taarifa za waathirika itatolewa kwa umma,” alisema. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles