TRAVEL START KUPELEKA WATANZANIA UGHAIBUNI KUPITIA KAMPENI YA KIJANJA

0
741

Brighiter Masaki – Dar es Salaam

Miss Tanzania 2004, Faraja Nyalandu na Mwanamuziki Grace Matata wamelamba dili la ubalozi wa Kampuni ya Usafiri wa Anga ya Travelstart katika kampeni ya kuwafikia wateja kwenye huduma zitolewazo na kampuni hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo jijini Dar, Meneja wa Travelstart, Robert Othman anasema wameamua kufanya kampeni hiyo ili kuweza kuwafikia wateja kwa haraka kutumia mitandao.

“Tumeamua kufanya kampeni hii kwa muda wa miezi miwili, kutakuwa na mashindano kwa watu wote, hii tumeona ni njia pekee ya kuwashukuru wateja wetu kwa kuwa nasi kwa kipindi kirefu.

“Kwenye matangazo yetu ya barabarani, endapo mtu akipita maeneo yenye matangazo yetu, akiona mdudu aina ya nyuki, kipepeo na konokono apige picha na atume kwenye mtandao wetu atakuwa amejipatia fursa ya kusafiri kwa gharama za kampuni yetu.

“Safari hizo kwa washindi watasafiri kwa muda wa siku mbili, kwa wale ambao watapata bahati ya kwenda nje ya nchi na nchi ambazo watakwenda ni Thailand, Jordan, Amsterdam, Dubai au Mauritius na kwa mikoa ya hapa tutaangalia huenda tukasafirisha kwenda labda Ngorongoro, Serengeti, Zanzibar na sehemu nyingine,” anasema meneja huyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here