24.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, March 28, 2023

Contact us: [email protected]

Trafiki waomba rushwa washtakiwa kwa Waziri Mkuu

                          Bethsheba Wambura Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigela afanye uchunguzi wa tuhuma za rushwa zinazowakabili

Askari wa Usalama barabarani wanaodaiwa kuwaomba rushwa madereva wa noah wilayani Lushoto wanaosafirisha abiria ndani ya wilaya hiyo na kisha awasilishe taarifa kwake leo Alhamisi Novemba Mosi.

Waziri Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni Jumatano Oktoba 31, baada ya kumkabidhi orodha ya  majina ya askari hao  yaliyowasilishwa kwake kupitia mabango ya wananchi alipokuwa  akihutubia mkutano wa hadhara katika uwanja wa Sabasaba, Lushoto mjini.

Mbali ya wananchi kuwasilisha malalamiko hayo pia mbunge wa Lushoto, Shaaban Shekilindi amemuomba Waziri Mkuu awasaidie kutatua kero hiyo inayowakabili wananchi.

Awali Waziri Mkuu alizungumza na watumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo katika ukumbi wa chuo cha Mahakama Lushoto.

“Serikali haina msamaha na mtumishi wa umma asiyetaka kufanya kazi kwa bidii na kuzingatia weledi, watumishi wa umma mnatakiwa kufanya kazi kwa kufuata maadili ya utumishi ili muweze kutimiza lengo la Serikali la kuwahudumia wananchi kwa kutumia taaluma zenu, “ alisema.

Waziri Mkuu ambaye alikuwa katika siku ya pili ya ziara yake ya kikazi mkoani Tanga alisema Serikali haina msamaha na mtumishi asiyetaka kubadilika na kufanya kazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,224FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles