Na Hadia Khamis, Mtanzania Digital
Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) imesema imeimarisha kasi ya mtandao wake ili kuwarahisishia wananchi kukamilisha malipo ya kodi kwa urahisi.
Hayo yameelezwa na Julai 11, 2022 na Ofisa Msimamizi Mkuu wa Kodi TRA, Peter Shewiyo kwenye maonyesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara maarufu kama Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa wananchi wengi waliofika Katika Banda hilo walikuwa wanalalamikia suala la mtandao.
“Tupo hapa katika maonyesho ya sabasaba tangu yalipoanza hadi leo kwa lengo la kutoa elimu kwa wananchi lakini pia kuwahudumia,” amesema Shewiyo.
Amefafanua kuwa wananchi walikuwa wanaulizia kuhusu mtandao nakwamba wameutengeneza wenyewe hivyo watataufanyia marekebisho.
Ameongeza kuwa wananchi wengi walifika kwa ajili ya kulipa kodi lakini pia kupata Stemp za Biashara.
“Wananchi ni wengi waliokuja kwenye banda letu, lakini tulipata wageni ambao walitaka kujua misamaha gani ya kodi wataipata kama wakiwekeza nchini,” amesema Shewiyo.
Aidha, amewataka wananchi kuendelee kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa .