29.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 20, 2024

Contact us: [email protected]

TRA yawataka wafanyabiashara Kilimanjaro kucha udanganyifu

Safina Sarwatt,Moshi

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Kilimanjaro imewataka wafanyabiashara kuacha tabia ya kutumia risiti moja kusafirisha bidhaa zaidi ya moja.

Akizungumza na wafanyabiashara wanaouza vifaa vya magari na pikipiki katika mkutano uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Umoja Hostel mjini Moshi, Msimamizi Mkuu wa (EFD’s) mkoa wa Kilimanjaro kutoka (TRA), Jerome Ndibalema amesema kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa na tabia ya kutumia risiti moja kusafirisha bidhaa ziadi ya moja.

Ndibalema amesema wako baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu wanaotumia risiti moja kusafirisha bidhaa zao hivyo kuikosesha serikali mapato, akiwashauri kuacha mara moja tabia hiyo.

“Changamoto tuliyonayo kwa sasa ni kwa baadhi ya wafanyabiashara kutumia risiti moja kusafirisha bidhaa zaidi ya moja na tatizo hilo haliko kwa mkoa wa Kilimanjaro pekee bali lipo kwa nchi nzima, lakini TRA iko nyuma yao inawafuatilia wafanyabiashara hao.

“Nawashauri wafanyabiashara waachane na mchezo huo, kwa sababu sheria imetungwa kwamba ni haki ya kila mteja na kila mnunuzi kupata risiti yake, na ni haki ya muuzaji kutoa risti kwa ajili ya Yule aliyemuuzia, vitendo wanavyovifanya vya kutumia risti moja kuwasafirishia mizigo zaidi ya moja sio vitendo sahihi,” amesema Ndibalema.

Nae Meneja Msaidizi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kilimanjaro upande wa madeni, Tilson Kabuje, amewahimiza wafanyabiashara kuhakikisha wanatunza kwa usahihi taarifa zao za ulipaji wa kodi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Wafanyabiashara Tanzania mkoa wa Kilimanjaro, Hillary Lyatuu, amepongeza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoa wa Kilimanjaro kwa kuwapatia elimu kuhusu wajibu na haki za mlipa kodi.

Aidha, amesema mkakati walionao kwasasa ni kuhakikisha kila mfanyabiashara anasajiliwa kwa mfumo wa kieletroniki ili aweze kutambulika zaidi, ambapo hadi sasa jumla ya wafanyabiashara 450 Manispaa ya Moshi wamesha sajiliwa katika mfumo wa kieletroniki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles