22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

TRA YAWAPIGA MSASA MADALALI WA BIMA

Meneja wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Diana Masalla
Meneja wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Diana Masalla.

Na Tiganya Vincent-MAELEZO-Dar es Salaam

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa mafunzo ya siku moja kwa Madalali wa Bima Tanzania yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kuifahamu vema Sheria ya Kodi ya Mwaka 2014 ili waweze kushiriki vema na kuondoa kasoro katika ulipaji wa kodi ya ongezeko la thamani kutoka sekta ya bima.

Kauli hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam na Meneja wa Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Diana Masalla wakati wa mkutano na waandishi wa habri kwenye semina ya siku moja kwa madalali hao ya kuwajengea uwezo kuhusu Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT).

Alisema kuwa mafunzo hayo yamewaelimisha wanachama hao juu ya kodi ya zuio, utoaji wa Kodi ya ongezeko la Thamani (VAT) na jinsi ya kulipa kwa njia ya mtandao.

Alisema kuwa TRA imekuwa ikitoa mafunzo hayo kwa wanachama na mawakala wa bima kwa sababu kabla ya Sheria ya Mwaka 2014 walikuwa halipi kodi na hivyo semina hiyo imesaidia wanachama hao kuwa na uelewa mpana juu ya ulipajji wa kodi ya ongezeko la thamani.

Kwa upande wa Mwenyekiti wa Chama cha Madalali wa Bima Tanzania,  Mohamed Jaffer aliipongeza TRA kwa hatua yake ya kutoa elimu kwa wanachama wake kwani imesaidia sana kuwajengea uwezo ambao utasaidia ulipaji wa kodi hizo.

Alisema hatua hiyo itasaidia kuondoa makosa katika masuala ya ulipajji kodi na jinsi ya ujazaji wa malipo ya kodi kwa wanachama wao.

Jaffer alisema kuwa ni muhimu sana wanachama hao kuelewa vema jinsi ya kujaza na kulipa kodi kwani asilimia 60 ya mapato ya bima yanatokana na madalali wa bima kwa kuwa wao ndiyo wako karibu na wateja kuliko Kampuni za Bima ambazo zinabaki na asilimia 40.

Alisema kuwa hadi hivi chama hicho kina wanachama wapato 150 ambao wamesambaa nchi nzima ambao kwa mwaka uliopita waliweza kukusanya wastani wa Sh bilioni 370.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles