27.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

TRA yawapa wafanyabiashara mbinu za kutunza kumbukumbu

KOKU DAVID-DAR ES SALAAM

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imewapa wafanyabiashara mbinu za namna ya kutunza kumbukumbu ili kuweza kufanikiwa katika biashara zao na kuiletea nchi maendeleo.

Akizungumza baada ya mkutano wao na Jumuiya ya Wafanyabiashara Taifa (JWT), Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Msafiri Mbibo, alisema kuwa ili kuweza kufanikiwa na kufikia malengo kila mfanyabiashara anatakiwa kutunza kumbukumbu za biashara zake  ili kudhibiti mwenendo wa shughuli anazofanya.

Alisema sambamba na hilo bila huduma ya umeme, maji, barabara, ulinzi na usalama pamoja na miundombinu mbalimbali biashara haziwezi kufanyika hivyo, TRA na wafanyabiashara ndio wanaoweza kufanikisha hayo kwa kuwa wazalendo katika suala zima la ulipaji na ukusanyaji wa kodi.

“Katika mkutano wa leo watafundishwa elimu ya utunzaji wa kumbukumbu za biashara zao zitakazowawezesha kudhibiti gharama zisizo za msingi katika biashara na zinazosababisha hasara ikiwa ni pamoja na masuala mbalimbali yanayohusu kodi kutokana na kuwa elimu haina mwisho kwa kila mtu’” alisema Mbibo.

Alisema baadhi ya wafanyabiashara wanapata hasara katika biashara zao kutokana na kutokutunza vizuri kumbukumbu za biashara zao hali inayopeleka kushindwa kuendelea na biashara hivyo TRA ina jukumu la kuwafundisha namna bora ya utunzaji wa kumbukumbu hizo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles