33.2 C
Dar es Salaam
Sunday, September 19, 2021

TRA YATOA MSAADA WALIOATHIRIKA NA MAJANGA

Safina Sarwatt, Kilimanjaro

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) mkoani Kilimanjaro, imekabidhi msaada wa vyakula kwa waathirika wa majanga ya mvua katika Kata ya  Ruvu wilayani Same mkoani Kilimanjaro, zilizosababisha wananchi zaidi 2,000 kukosa makazi.

Akitoa msaada huo Meneja wa TRA Mkoa wa Kilimanjaro, Msafiri Mbibo, amesema mamlaka imeona umuhimu wa kushirikiana na jamii ili kuwanusuru waathirika hao.

Mbibo amesema misaada ambayo ni mchele kilo 330 na maharage kilo 140, ni sehemu ya huduma na kwamba wataendelea kuchangia ili kuwanusuru waathirika hao wa majanga ya mvua.

“Kwa sasa tumeona tutoe mahitaji ya muhimu ya  chakula kwa sababu na sisi ni sehemu ya jamii hivyo tutaendelea kushirikiana na Mkuu wa Mkoa, kuhakisha wananchi walipatwa na majanga wanakuwa salama,” amesema.

Akipokea msaada huo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Anna Mghwira, amesema zaidi ya tani 11 za mahindi na tani 5.6 za maharage zinahitajika kwa ajili ya waathirika hao.

 

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
156,882FollowersFollow
518,000SubscribersSubscribe

Latest Articles