26.5 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 26, 2023

Contact us: [email protected]

TRA yakutana na viongozi wa dini

Yeremiah MbaghiNA KOKU DAVID, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imekutana na wadau mbalimbali wa taasisi za dini ya kikristu katika semina ya siku moja iliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwaelimisha kuhusiana na sheria mpya ya kodi.

Akizungumza baada ya semina hiyo, Kaimu Meneja Elimu kwa Mlipa Kodi, Yeremiah Mbaghi, alisema kuwa sambamba na kuwapa elimu ya kod pia wamekutana nao ili kupata mrejesho kutoka kwao kutokana na huduma wanazozipata ndani ya mamlaka.

Alisema kuwa wamekutana na wadau hao wa taasisi ya dini ili kuwaelimisha kuhusiana na mabadiliko ya sheria ya VAT ya mwaka 1997 ambayo katika usajili ilikuwa inamtaka mtu yeyote mwenye mapato au mauzo ya kuanzia milioni 40.

“ Lakini kutokana na mabadiliko ya sheria mpya ya mwaka 2014 ambayo inatumika sasa, inamtaka mtu mwenye mapato ya kuanzia milioni 100 na kuendelea ndiye asajiliwe,” alisema.

Alisema pia wanawafundisha ili kujua wajibu wao kwa serikali ikiwa ni pamoja na kupokea maoni yao iwapo wanahitaji mabadiliko au kuboreshewa huduma kama kutakuwa na uhitaji huo.

“Hapa tunaelimishana kuhusiana na sheria ikiwa ni pamoja na kukumbushana wajibu, kufuata sheria na taratibu lakini changamoto tunayokutana nayo ni baadhi ya watu kutojua kwamba baada ya kusajiliwa katika taasisi nyingine pia wanatakiwa kusajiliwa na TRA hivyo ndio maana tupo hapa kuelimishana zaidi katika mambo mbalimbali yanayohusiana na TRA,” alisema Mbaghi.

Naye Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Exebius Nzigilwa, alisema kodi sio kitu kigeni kwa kanisa na kwamba kanisa katoliki litashirikiana na Serikali katika kuhakikisha inalipa kodi kwa hiyari kwa mujibu wa sheria katika sehemu zote zinazotakiwa.

“Kadri tutakavyopata elimu ya kodi tutatimiza wajibu wetu kwani hata Bwana wetu Yesu Kristu alitambua umuhimu wa kodi na alifanya kazi na watoza ushuru ambao miongoni mwao walikuwa wanafunzi wake,” alisema Askofu Nzigilwa.

Kwa upande wake Ofisa Uhusiano wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Cletus Majani, alisema mtu yeyote anayeingiza nchini vitu vyake binafsi kupitia taasisi ya dini kwa lengo la kukwepa kodi huyo ni mwizi na kwamba sheria zichukuliwe dhidi yake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,726FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles