27.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 20, 2023

Contact us: [email protected]

TRA yakusanya Sh trilioni 15.9 kwa miezi 12

Mwandishi wetu-Dar es salaam

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imetangaza kuwa imekusanya Sh trilioni 15.9 kati ya lengo la kukusanya Sh trilioni 18 kwa mwaka wa fedha 2018/19.

Taarifa kwa umma iliyotolewa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Richard Kayombo, makusanyo hayo ni ya kati ya Julai mosi mwaka jana hadi Juni 30, mwaka huu.

“Aidha, katika robo ya nne ya mwaka huo wa fedha, yaani mwezi Machi hadi Juni 2019, TRA ilikusanya Sh trilioni 1.1, Sh trilioni 1.2 na Sh trilioni 1.5 kwa mwezi Aprili, Mei na Juni. Kwa namna ya kipekee kabisa, TRA inawashukuru walipakodi na wananchi wote kwa ujumla kwa ushirikiano,” ilisema taarifa hiyo.

Ilisema katika mwaka huo wa fedha, Serikali ilianzisha Mfumo wa Stempu za Kodi za Kielektroniki (ETS) ambao utekelezaji wake umefanyika kwa awamu mbili.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, awamu ya kwanza ilihusisha bidhaa za sigara, mvinyo, pombe kali, bia na aina zote za vileo.

Kwamba katika awamu hiyo iliyoanza kutekelezwa Januari 15, mwaka huu, imeendelea vizuri na maandalizi ya awamu ya pili ya utekelezaji wa ETS inayojumuisha bidhaa za vinywaji baridi, maji, juisi, na CD/DVDs yamekamilika.

“Hivyo mfumo huu wa ETS kwa awamu hii ya pili unatarajiwa kuanza kazi Agosti Mosi (leo). Lengo kuu la kubandika stempu hizi za kielektroniki ni kuongeza usimamizi na ufanisi wa ukusanyaji wa ushuru wa bidhaa, ikiwa ni pamoja na kupata taarifa sahihi za uzalishaji viwandani ili kukusanya mapato stahiki.

“Ni matumaini ya TRA kuwa wazalishaji, waingizaji, wasambazaji, wauzaji wote wa bidhaa zinazotozwa ushuru wa bidhaa pamoja na umma kwa ujumla, wataendelea kutoa ushirikiano kwa TRA ili kufanikisha utekelezaji wa mfumo huu kwa kila mmoja kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo,” ilisema taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
210,784FollowersFollow
563,000SubscribersSubscribe

Latest Articles