26.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

TRA yakamata DVD bandia zenye thamani ya bilioni 1/-

pic+TRANA HERIETH FAUSTINE

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imekamata CD na DVD 650,000 zenye thamani ya Sh bilioni moja kwa ukwepaji wa kodi.

Pia katika zoezi hilo mitambo 47 ya kudurufu CD na DVD pamoja na kompyuta nne zimekamatwa.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu ya Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo, alisema bidhaa hizo zilipatikana baada ya  kuwepo kwa msako mkali ulioshirikisha wadau wa tasnia ya muziki na filamu.

Alisema baada ya kukokotoa kupitia gharama ya ushuru wa bidhaa hizo  waligundua kuwepo kwa upotevu wa Sh milioni 31 na milioni 11  ambazo zilikuwa ni gharama za stempu zilizotakiwa kubandikwa katika CD na DVD  hizo.

“Makampuni yanayoshiriki katika uuzaji wa kazi hizo kinyume na sheria ni Kilimanjaro house music, Oneshop, Siku hazifanani DVD, roommate technology, fety big star wanaofanya kazi hizo eneo la Kariakoo,” alisema Kayombo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles