27.9 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

TRA yajipanga kukusanya Sh trilioni 12

Richard Kayombo
Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo

Na Arodia Peter, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) inatarajia kukusanya Sh trilioni 12 katika mwaka wa fedha 2014/2015 endapo itapata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa Serikali pamoja na walipa kodi.

Akizungumza na gazeti hili hivi karibuni, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo, alisema katika mwaka wa fedha 2013/ 2014, TRA ilikusanya jumla ya Sh trilioni 10.3 kutoka trilioni 8.04 mwaka 2012/2013 hivyo wana imani hata kiwango hicho cha sasa kitafikiwa.

“Lengo letu ni kuongeza juhudi na kukusanya Sh trilioni 12 kwa mwaka huu wa fedha, lengo hili litafikiwa endapo tutaziba mianya ya ukwepaji kodi na kutoa elimu zaidi kwa walipa kodi.

Katika hatua nyingine, mkurugenzi huyo alisema TRA imeanzisha mfumo mpya wa kiforodha ujulikanao kama ‘Tansis’ wenye lengo la kupunguza usumbufu kwa wafanyabiashara wanaotoa mizigo katika Bandari ya Dar es Salaam na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere.

Alisema huduma hiyo ni maboresho ya huduma ya awali iliyokuwa ikijulikana kama asycuda ++ ambayo ilikuwa inasababisha usumbufu katika utoaji wa mizigo.

Akifafanua zaidi kuhusu mfumo huo, Kayombo alisema mfumo huo pia utawezesha wafanyabiashara na mawakala kupata taarifa za mizigo yao pamoja na malipo wanayopaswa kulipa TRA kupitia simu zao za mkononi.

Kayombo alibainisha kuwa mfumo wa Tansis umeonyesha mafanikio makubwa katika upokeaji wa mizigo tangu ulipoanza kwa majaribio mkoani Dar es Salaam Aprili mwaka huu kwa kampuni kubwa 13.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles