28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TRA KUUNGANISHA MASHINE EFD NCHINI KUPUNGUZA BEI

Na KOKU DAVID-DAR ES SALAAM                  |              


SERIKALI imeweka mpango mkakati kuhakikisha mashine za kutolea risiti za kodi za kielektroniki (EFD), zinatengenezwa hapa nchini ili kuwarahisishia wafanyabiashara kuzipata kwa gharama nafuu.

Sambamba na hilo, pia imepunguza Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwenye mashine za EFD ili kumwezesha kila mfanyabiashara kuweza kuzinunua na kuzitumia.

Lengo la Serikali ni kumrahisishia mfanyabiashara katika utunzaji wa kumbukumbu za biashara zake pamoja na kuwezesha kodi yake stahiki iweze kufika bila usumbufu lakini pia kila mfanyabiashara anayestahili kulipa kodi alipe.

Awali kabla ya punguzo la kodi ya Ongezeko ya Thamani (VAT), mashine za EFD zilikuwa zikiuzwa kwa shilingi 690,000 lakini hivi sasa zinauzwa shilingi 590,000.

Katika kuhakikisha elimu ya kodi inamfikia kila mwananchi, mamlaka hiyo hivi karibuni ilishiriki katika maonyesho ya 25 ya Sikukuu ya Wakulima ya Nanenane ambayo kitaifa yalifanyika katika viwanja vya Nyakabindi mkoani Simiyu Wilaya ya Bariadi ambako wananchi pamoja na wafanyabiashara mbalimbali walitembelea banda la TRA na kupata elimu mbalimbali ya masuala ya kodi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles