23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TRA Kagera yapongezwa Kwa utendaji kazi mzuri licha ya mlipuko wa corona

Mackdonald Mwakasendile – Kagera

Mamalaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoani kagera imepongezwa kwa kuendelea kufanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato kwenye mipaka ya nchi zinazopakana na mkoa huo licha ya uwepo wa changamoto ya ugonjwa wa corona uliopelekea baadhi ya nchi jirani kufunga mipaka yake.

Hayo yamezungumzwa na Naibu Kamishna Mkuu wa mamlaka hiyo, Msafiri  Mbibo wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani kagera .

Amesema katika mpaka wa Mtukula walilenga kukusanya mapato ya shilingi bilioni 15.5 lakini wameweza kuvuka lengo kwa kukusanya shilingi bilioni 19.5, hali ambayo imeonyesha ni kwa kiasi gani corona ambavyo haijaathiri shughuli za ukusanyaji wa ushuru katika mpaka huo unaopakana na nchi ya Uganda kwa Tanzania.

Amesema kuwa pia katika ushuru wa ndani bado mamlaka hiyo imeendelea kufanya vizuri katika maeneo mbalimbali hapa nchini, jambo ambalo ametumia fursa hiyo kuwashukuru wafanyabisha na wananchi kwa kumuunga mkono Rais Magufuli katika kulipa kipaumbele sual la ulipaji Kodi.

” Mwitikio wa wananchi katika kulipa kodi kwa hiyari bila kushurutishwa kama ilivyokuwa miaka ya nyuma inaonyesha ni kwa kiasi gani wananchi wa nchi hii, hususani wafanyabiashara wanavyoipenda nchi yao na uongozi wa Rais Magufuli”. Amesema Mbibo.

Aidha amewataka wafanyakazi wa mamlaka hiyo hapa nchini kuendelea kuweka mahusiano mazuri kati yao na wafanyabiashara kwa kusikiliza kero zao au malalamiko yanayohusu ulipaji kodi na kuangalia ni kwa namna gani wanaweza kuzitatua.

Amesema kuwa sambamba na suala hilo, ameitaka mamlaka hiyo mkoani Kagera kuwaeleza wafanyabiashara ni kwa namna gani wanavyoweza kushiriki minada inayoendeshwa na mamlaka hiyo kwa njia ya mtandao na faida zake ili kuwawezesha kunufaika na ununuzi wa bidhaa zinazokuwa zinauzwa na mamlaka hiyo ikiwemo magari na bidhaa nyingine .

Amesema kuwa inaonyesha bidhaa nyingi zinazonunuliwa hapa mkoani kagera ambazo zinakuwa kwenye minada ya TRA hununuliwa na wafanyabiashara au matajiri kutoka mikoa ya Dar es Salaam, Mwanza na Dodoma hali ambayo inaweza ikawa inasababishwa na wafanyabiashara hao kutokuwa na  uelewa wa juu ya minada inayoendeshwa na mamlaka hiyo kwa njia ya mtandao.

“Inatakiwa uongozi wa mkoa utumie radio za kijamii kuwaeleza wananchi na wafanyabiashara namna tunavyoendesha minada hii na faida zake”, amesema Mbibo.

Amesema kuwa endapo wafanyabiashara na wananchi wa mkoa wa Kagera wataelewa jambo hili mwitikio wa ushiriki wa mnada kwa wananchi utaongezeka.

Amesema kuwa ziara yake ni ya kawaida ambapo ametembelea mpika ya Mtukula, Rusumo na Kabanga iliyopo mkoani Kagera ikiwa ni pamoja na kuzungumza na watumishi wa mamlaka hiyo waliopo katika mkoa wa huo katika vikao vya ndani.

Amesema ziara hiyo itaendelea katika mikoa yote ya Tanzania na kwamba lengo ni kuona namna  watumishi wa mamlaka hiyo wanavyofanya kazi na changamoto zilizopo mikoani katika mamlaka ili ziweze kutatuliwe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles