25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

TPSC KUIMARISHA WATUMISHI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki

Na JONAS MUSHI -DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Angellah Kairuki, amesema Serikali kupitia Chuo Cha Utumishi wa Umma (TPSC) itaendelea kuwajengea uwezo watumishi wa umma ili waendane na kasi ya mabadiliko, changamoto na mahitaji ya sasa katika utumishi wa umma.

Akiwasilisha taarifa ya chuo hicho kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Utawala na Serikali za Mitaa Dar es Salaam jana, Waziri Kairuki alisema mafunzo hayo ni muhimu kwa watumishi.

Aliongeza kuwa Serikali inakamilisha mchakato wa maandalizi ya mafunzo ya lazima kwa watumishi wa umma nchini.

Katika kuongeza ufanisi na tija, chuo hicho kimejenga, kuhuisha na kusimika mifumo mbalimbali ya kusimamia utekelezaji wa majukumu.

“Baadhi ya mifumo hiyo ni mpango mkakati wa mwaka 2016-2021, utekelezaji kikamilifu wa mkataba wa huduma kwa mteja na kuanzishwa kwa dawati la malalamiko na kamati za uadilifu.

Aidha Kairuki aliyataja majukumu mengine kuwa ni kuendelea kusimika mifumo ya tehama, miundombinu ya mtandao (LASN), mtandao wa Serikali (Govnet), mfumo wa simu za Serikali (Voip) na mfumo wa barua pepe za Serikali (GSM).

Waziri Kairuki aliiambia kamati hiyo kuwa katika kuendeleza weledi wa watumishi wa umma kwenye utunzaji wa kumbukumbu na uhazili, chuo kinatarajia kuanzisha shahada ya kwanza kwenye maeneo hayo mawili.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Utawala na Serikali za Mitaa, Jasson Rweikiza, alikipongeza chuo hicho kwa jitihada zake za kuwaendeleza watumishi wa umma na kutoa ushauri kwa Serikali ili ifungue tawi la chuo hicho jijini Mwanza kuwahudumia wakazi wa Kanda ya Ziwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles