Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
MAMLAKA ya Afya ya Mimea na Viuatilifu (TPHPA) Kanda ya Mashariki, imegawa miche ya matunda katika Shule za Sekondari za Diplomasia, Uhamiaji, Mwalimu Nyerere na Kiungani zilizopo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza leo Juamosi Machi 9, 2024 kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPHPA, Profesa Joseph Ndunguru, Meneja wa Kanda ya Mashariki, Dk. Mahamudu Sasamalo alisema wamegawa jumla ya miche 60 ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan za kutaka Watanzania watunze mazingira kwa kupanda miti.
“Sisi kama TPHPA tumeamua kutoa miti ya matunda na hasa mashuleni kwa kuhakikisha kuwa watoto wetu wanapata hewa safi, kivuli na zaidi wapate matunda,” amesema Dk. Sasamalo.
Amesema TPHPA inaendelea na jitihada za kutunza mazingira kwa vile afya ya binadamu na wanyama ni miongoni mwa jukumu lao.
“Lakini sote tuna wajibu wa kutunza mazingira na kupanda miti, ina faidi nyingi sana,” amesema Dk. Sasamo.