29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 6, 2023

Contact us: [email protected]

TPDC yatumia zaidi ya milioni 246 katika shughuli za maendeleo

PATRICIA KIMELEMETA

Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC) katika kuendeleza mradi wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) wameweza kutumia zaidi ya Sh. milioni 246 kugharamia shughuli mbalimbali za maendeleo nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo Jumatano Mei 22, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika hilo Mhandisi Kapuulya Musomba amesema kuwa fedha hizo zimetumika katika vipindi tofauti ili kuhakikisha wananchi wanapata maendeleo na kunufaika na rasilimali zao.

Amesema katika fedha hizo, shirika hilo liliweza kuchangia ujenzi wa miundombinu ya kusambaza maji safi  yenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 21 katika eneo la Songosongo lililopo Kilwa Mkoani Lindi.

“Katika kipindi hiki ambacho tunasheherekea miaka 50 tangu kuanzishwa kwa TPDC, kuna miradi mbalimbali ambayo tumeifanya kwa jamii ili kuhakikisha wananchi wananufaika na rasilimali zao,” amesema Musomba.

Ameongeza kuwa miradi hiyo ni pamoja na wa maji uliotekelezwa katika Kijiji cha Kilangala B kilichopo Mkoani Lindi, wenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 52

Miradi mingine ni ile ya ujenzi wa madarasa katika Halmashauri ya Mtwara yenye thamani ya Sh. milioni 13 na ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Kibibi Bunju B wenye thamani ya Sh milioni 10.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles