25.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

TPDC YASAMBAZA GESI KWA WATEJA 1,000 DAR

CHRISTINA GAULUHANGA Na TUNU NASSOR


SHIRIKA la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limesema hadi sasa limeanza kusambaza gesi nyumbani kwa wateja 1,038 wa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na MTANZANIA jana jijini Dar es Salaam, katika Maonyesho ya 47 ya Sabasaba, Mhandisi Limi Lagu kutoka TPDC, alisema katika kutekeleza mpango huo, wameingia mkataba na kampuni tanzu ya Gasco, ambayo ndiyo inayofunga mitambo, inaendesha na kufanya ukarabati.

Alisema mpaka sasa nyumba 38 za Mikocheni zimefikiwa na mradi huo, huku wakiendelea kuwafungia wateja wengine 1,000.

Alisema wateja hao 1,000 wanatoka maeneo ya Mwenge, Ubungo, Sinza, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Tegeta.

Limi alisema pia wamelenga kuwaunganishia wateja 850 wa Mkoa wa Mtwara na Lindi.

“Wateja wa awamu hii ya kwanza wananufaika na gesi hii baada ya mifumo ya gesi kupita maeneo yao ambapo tumekuwa tukishirikiana pia na uongozi wa serikali za mitaa kwa ajili ya kuwapa elimu juu ya umuhimu wa matumizi ya gesi asilia.

“Hadi Juni 2019, tunataka tuwe tumewafikia wateja 1,850, malengo yetu ni wananchi kunufaika na gesi yao,” alisema Lagu.

Alitaja mikoa itakayofikiwa na mradi huo kuwa ni Tanga, Pwani, Dodoma na Dar es Salaam.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles