TPDC YASAIDIA UJENZI WA ZAHANATI TANGA

0
779

Na Editha Karlo, Lushoto

Shirika la Maendeo ya Petroli Tanzania (TPDC), imekabidhi hundi ya Sh milioni nne ili kusaidia  ujenzi wa Zahanati ya kijiji cha Kidunda Wilayani Lushoto Mkoani Tanga.

Akikabidhi mfano wa hundi kwa Mwenyekiti wa Kijiji kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa TPDC, Asia Mrutu ambaye amesema mchango huo umetokana na maombi ya serikali ya kijiji kwa TPDC kusaidia jitihada za  ujenzi wa zahanati hiyo.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Kidundai, baada ya kukabidhiwa hundi hiyo amesema fedha hizo zitawezesha ununuzi wa nondo 40 zenye futi 40 kila moja, mifuko ya saruji na matofali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here