26.9 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

TPDC yang’ara mashindano ya Shimuta, yaichapa TBS

Na MWANDISHI WETU

TIMU ya Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) leo wameibuka na ushindi wa seti 2-0 katika mchezo wa kuvuta kamba dhidi ya timu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) katika muendelezo wa michuano ya Shimuta inayoendelea Jijini Tanga.

Kwa upande wa wanaume walivuta kamba na chuo cha DIT jana na kupata seti 2-0 na leo wamevuta na chuo cha IAA na kupata mivuto 2-0 na wanaamini mechi zilizobaki wataendelea kushinda na kutinga hatua ya fainali.

TIMU ya Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC) ambao waliigaragaza TBS set 2-0 kwenye mchezo wa kuvuta kamba uliofanyika kwenye viwanja vya shule ya Sekondari Popataly Jijini Tanga wakiwa kwenye picha ya pamoja

Mchezo huo wa uliochezwa kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Popatlal Jijini Tanga leo ulionekana kuwa na upinzani lakini TPDC ambao walikuwa wamesheheni wachezaji mahiri na wenye viwango waliweza kuwagaragara wapinzani wao.

Akizungumzia ushindi huo na namna walivyojipanga kuelekea kwenye michezo yao mengine,Kocha wa timu hiyo Joram Ndalalwa alisema timu hiyo imejipanga vizuri kunyakua ubingwa kwenye michuano hiyo.

Joram alisema kila wakati mara baada ya kumalizika kwa mchezo mmoja wanarudi kujitafakari na kujipanga upya kuona namna ya kujiandaa vema .

Alisema baada ya kumalizika mchezo huo na kuweza kuibuka na ushindi wanarudi kujipanga kwa ajili ya mchezo wao unaofuata dhidi ya ATC utakaochezwa Novemba 23 mwaka huu asubuhi na jioni watapambana na UDSM.

Akizungumzia mashindano hayo Katibu wa Michezo kutoka TPDC Elinaike Naburi alisema kwamba walishiriki mashindano hayo ya shimuta mwaka huu ikiwa ni mara yao ya tano mpaka sasa wamekwisha kushiriki michezo wa mpira wa miguu,wavu,pete,kikapu pamoja na michezo ya Jadi,Karata,Table na Draft.

Alisema mchezo wa vishale watamaliza kuanzia Novemba 24 na 25 watafanya mbio mpaka sasa wamefanikiwa kutinga hatua ya 16 katika mpira wa miguu na Pete waliishia kwenye makundi kwa kuwa mshindi wa tatu huku Wavu wakiishia kwenye makundi lakini walionyesha ushindani mkubwa.

Kikapu waliishia kwenye makundi lakini ushindano wao ulikuwa wa hali ya juu katika michezo ya jadi wameshinda kwa kuwa mabingwa karata upande wa wanawake na mshindi wa pili upande wa wanaume.

Katika mchezo wa drafti alisema waliishia hatua ya robo fainali upande wa wanaume huku wanawake wakiishia hatua za makundi na mchezo wa Pooltable wanawake wamefanikiwa kutetea taji lao kwa kuwa mshindi wa pili mwaka jana mshindi wa kwanza na wanaume waliishia nusu fainali.

Alisema kwamba katika mchezo wa bao wachezaji wao wote wameishia hatua ya nusu fainali huku akieleza malengo ya mashindano hayo kwa TPDC ni kuonyesha ushindani wa hali ya juu.

Alisema pia malengo yao ni kuweza kufahamiana na Taasisi nyengine kujenga mshikamano kama wafanyakazi na kuendelea kutoa morali na motisha kwa wafanyakazi kuendelea kushiriki michezo kwa sababu ni afya.

Hata hivyo alisema wamefurahi kupata nafasi ya kushiriki mashindano hayo na wanaamini wametoa ushindani wa kutosha na wataendelea kufanya hivyo michezo yao iliyobaki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles