25.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

TPDC yajenga visima, uzio wa shule Lindi, Mtwara

Florence Sanawa, Mtwara na Hadija Omary, Lindi

Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), imezipiga tafu mikoa ya Lindi na Mtwara kwa kuwajengea visima vya maji na uzio wa shule.

Msaada huo unazihusu Shule ya Ufundi Mtwara ambapo imejengewa uzio kwa gharama ya Sh milioni 59 huku Lindi ikikabidhiwa Sh milioni 52.3 kwa ajili ya mradi wa maji katika Kijiji cha kilangala B, Halmashauri ya Mtama.

Akikabidhi msaada huo mkoani Mtwara, Mkurugenzi Mkuu wa TPDC, Dk. James Mataragio amesema wametoa ili kuchangia ujenzi huo kwani kwa kiasi kikubwa itachangia kuunga mkono juhudi za serikali.

“Tumetoa Sh milioni 50 ili kuchangia kujenga ukuta wa shule ambao kwa kiasi kikubwa umekuwa ni msaada mkubwa pia tumefanikiwa kujenga shule, kutoa vitabu na  kusaidia miundombinu mbalimbali kama vile kutoa elimu kwa shule mbalimbali ambapo tuna klabu 32 za mafuta na gesi, hii ni muhimu kwa wanafunzi na sekta hii ndiyo kwanza imeanza,’’ amesema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Rhoda Ngoka amesema ujenzi wa ukuta huo utasaidia katika malezi na usalama wa watoto katika shule hiyo huku akilishukuru shirika hilo kwa kuona umuhimu wa jambo hilo shuleni hapo.

Aidha, akizungumza mkoani Lindi wakati wa makabidhiano hayo, Dk Mataragio amesema fedha hizo ni kwa ajili ya malipo ya wakandarasi wa Kampuni ya J&M Fast Engineering ambapo fedha hizo zimeingizwa kwa awamu mbili awamu ya kwanza iliingizwa Sh milioni 25 na awamu ya pili Sh milioni 27.3.

“Tangu shirika hili limeanzishwa na kuanza kufanya kazi ya utafiti na uchimbaji wa gesi, limekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha tunasaidia jamii katika maeneo yaliyopitiwa na mradi huu katika sekta mbalimbali ikiwamo elimu, maji na afya kwa kutoa elimu au msaada wa kifedha ambapo kwa Mkoa wa Lindi pekee hadi sasa tayari tumefanikiwa kutoa Sh milioni 102 katika sekta ya afya na elimu,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles