23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 2, 2023

Contact us: [email protected]

TPDC yaeleza sababu ya mradi wa LNG kuchukua muda mrefu

Na Mwandishi Wetu, Lindi

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limeeleza sababu za kuchukua muda mrefu kwa mradi wa kusindika gesi asilia kuwa kimiminika (Liquefied Natural Gas-LNG) kuwa ni pamoja na zoezi la upitiaji wa mikataba.

Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani (Katikati) akiwa na wafanyakazi wa Wizara hiyo pamoja na Manejimenti ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Akizungumza kwenye kikao kilichokutanisha Wizara ya Nishati na wadau wa mradi huo, Mkurugenzi TPDC, Dk. James Mataragio amesema Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liliiagiza Serikali kufanya mapitio ya mikataba ya ugawanaji mapato (Production Sharing Agreement- PSA).

“Sababu zilizopelekea mradi kuchukua muda mrefu ambazo ni pamoja na zoezi la upitiaji wa mikataba ambapo bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liliiagiza serikali kufanya mapitio ya mikataba ya ugawanaji mapato (Production Sharing Agreement- PSA).

“Zoezi la kupitia mikataba ya PSA lilitekelezwa na ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali na lilipelekea majadiliano yaliyokuwa yameanza mwaka 2016 kusimama kupisha zoezi hilo muhimu kukamilika,” alisema Dk. Mataragio.

Upande wake, Waziri wa Nishati, Dk. Medard Kalemani akizungumza kwenye mkutano huo alieleza kuwa serikali imedhamiria kwa dhati kuteleleza mradi wa LNG na tayari kazi mbalimbali zimekwishafanyika ikiwemo utwaaji wa ardhi ya mradi yenye ukubwa wa hekta 2,071, ulipaji wa Sh bilioni 5.7 kama fidia kwa wananchi watakaopisha mradi huo.

“Upembuzi wa awali wa kihandisi (Pre FEED) pamoja na kuundwa kwa timu ya serikali ya majadiliano (Government Negotiation Team-GNT) na tiTimu ya wataalam (Technical Team) itakayofanya kazi na GNT.

“Serikali imejipanga kukamilisha majadiliano ya mkataba wa nchi hodhi (Host Governmemt Agreement-HGA) ndani ya miezi sita ili kuwezesha utekelezaji wa mradi kuanza mapema. Kufikia Oktoba majadiliano ya HGA yatakuwa yamekamilika,” alieleza Waziri Kalemani.

Aidha, Dk. Kalemani pia aliilekeza TPDC kukamilisha ndani ya mwezi mmoja zoezi la uwekaji wa mipaka katika eneo la mradi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,250FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles