27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, November 7, 2024

Contact us: [email protected]

TPDC KUUNGANISHA GESI KWA WANANCHI 350,000

CHRISTINA GAULUHANGA NaMARY KABORA (TUDARCO), DAR ES SALAAM



Shirika a Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), limesema limejipanga kuhakikisha ndani ya miaka mitatu litakuwa limewafikia wananchi 350,000 kwa kuwaunganishia nishati ya gesi asilia katika nyumba.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba, uunganishwaji huo utakwenda sambamba na kuunganisha viwanda mbalimbali vilivyopo hapa nchini.

“Uunganishaji huo wa gesi ni hatua za mafanikio zinazoendelea kufanywa na Shirika la Maendeleo ya Petroli nchini (TPDC), ambapo kwa sasa viwanda zaidi ya 40, zikiwamo nyumba mbalimbali jijini Dar es Salaam zimeunganishiwa nishati hiyo,” alisema Musomba.

Alisema tayari amefanya ukaguzi katika eneo linalowekwa toleo maalumu kwa ajili ya uunganishaji wa gesi asilia katika viwanda mbalimbali wilayani Mkuranga, Mkoa wa Pwani.

Alisema eneo hilo linalohusisha utoboaji wa bomba kubwa la gesi linalotokea Mtwara hadi jijini Dar es Salaam lenye urefu wa kilomita zaidi ya 550 linaongozwa na TPDC kupitia wataalamu wa shirika lake tanzu la kulinda miundombinu ya gesi (GASCO) kwa kushirikiana na Mkandarasi, China Petroleum Pipeline Engineering (CPPE).

Musomba alisema kuanzia sasa, TPDC ipo tayari kuunganisha nyumba na viwanda katika maeneo mbalimbali ambapo kadri maombi yatakavyowasilishwa kwao wapo tayari kufanya kazi.

Alisema gharama za uunganishwaji wa huduma ya gesi asilia kwa wananchi itategemea na ramani ya nyumba husika pamoja na umbali wa nyumba kutoka ilipopita miundombinu la bomba la gesi asilia linalotumika kusambaza katika maeneo ya makazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles