30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

TPB: UAMUZI WA KUUNGANISHA BENKI HAUTAKUWA NA MADHARA MAKUBWA

Na ASHA BANI – DAR ES SALAAM


OFISA Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania TPB Plc, Sabasaba Moshingi, amesema uamuzi wa kuunganishwa kwa benki tatu katika kipindi cha mwaka mmoja hautakuwa na madhara makubwa.

Moshingi aliyasema hayo jana, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi mwingine mpya wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kuridhia muunganiko wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB) na TPB.

Mei 17, Benki ya Posta iliunganishwa na Benki ya Twiga Bancorp na sasa Benki ya Wanawake, ambapo Ofisa Mtendaji huyo alisema wamejipanga na wanaendelea kujipanga ili wasiyumbe katika kuziendesha.

“Kama ilivyokuwa kwa Benki ya Twiga Bancorp, iliyounganishwa na benki yetu mwezi Mei mwaka huu, wafanyakazi, wateja, amana pamoja na rasilimali zote za Benki ya Wanawake nazo zitahamishiwa kwetu na naahidi tutafanya kazi vizuri.

“Naishukuru Serikali kwa kuendelea kuamini Benki ya TPB pamoja na Menejimenti yake kwa mara nyingine tena…nawahakikishia wateja wote waliokuwa na amana zao kwenye benki ya TWB wasiwe na wasiwasi kwa kuwa ziko salama,’’ alisema Moshingi.

Moshingi ameahidi kuendeleza lengo la uundwaji wa TWB katika kuwakomboa wanawake kwa kuwapatia elimu kuhusu masuala ya fedha na kisha kuwawezesha kwa kuwapatia mikopo, ili waweze kujiimarisha kiuchumi.

“Tutaendelea kutoa huduma maalumu kwa ajili ya wanawake kama ilivyokuwa lengo la TWB kwa kuweka dirisha maalumu la kuwahudumia kwenye matawi yetu nchini kote,’’ alisema Moshingi.

Aliongeza kuwa, kupitia dirisha hilo  maalum, wanawake wataweza kupata huduma zote za kibenki, hususan mikopo ya vikundi, Vicoba na hata mikopo binafsi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles