21.2 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

TPA: Ziwa Tanganyika ni lango la uchumi

Na MWANDISHI WETU-KIGOMA

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imesema  lango la uchumi nchini lipo Ziwa Tanganyika kutokana na ziwa hilo kupakana na nchi tatu zenye utajiri Afrika.

Kutokana na hali hiyo, imesema  thamani ya madini yaliyopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), unaofikia Dola za Marekani trilioni 24, zinahitaji usafirishaji wa uhakika kufika katika soko la dunia.

Akizungumza mjini Kigoma jana, Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Percival Salama, alisema Bandari za Ziwa Tanganyika zipo mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa kwa upande wa Tanzania.

Ziwa hilo, limepakana na nchi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Zambia na Burundi.

“Kama unatafuta asilimia ya kila nchi Ziwa Tanganyika, Tanzania ina asilimia 45, DRC 41, Burundi asilimia 8 na Zambia asilimia 6.

“Ni sahihi na vema kwa serikali za nchi hizi,zinapofanya uwekezaji wa miundombinu ya bandari  na vyombo vya usafirishaji kuhakikisha wananchi wa nchi hizo wanapata huduma.

“Tumelala kwenye utajiri wa kutupwa,tupo  Tanzania kwenye ukanda wenye utajiri wa kutupwa duniani sio tu Afrika.

“Unazungumzia Tanzania kama nchi tajiri kama anavyosema mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli mara nyingi,  Watanzania tunajua  Tanzania ni tajiri na kilichobaki ni fikra kuitumia vizuri ili kutumia vizuri fursa ile ya utajiri tulikuwa nao kubadilisha maisha ya nchi yetu kiuchumi pamoja na wananchi wake,” alisema

Alisema  DRC, ina utajiri wa madini na takwimu zinaonyesha utajiri wake ni Dola za Marekani trilioni 24 kupitia madini.

 “Na njia pekee ya kufikia soko la dunia, lazima upite Tanganyika uvuke Tanzania uende aidha kwenye bandari ya Dar es Salaam au Tanga ili uweze kufikia kwenye soko la dunia.  Kwa hiyo utaona kwa kifupi kilichobaki kwetu sisi Watanzania ni kujenga miundombinu sahihi, kujenga taratibu nzuri, kuweka mazingira rafiki ya kibiashara ambayo yatawafanya dunia iende Kongo na Kongo iende duniani,” alisema

Alisema katika suala la utendaji wa Bandari za Ziwa Tanganyika kuanzia mwaka wa fedha 2014/15, 16 mpaka 17/18 na 2018/19  kuna mtiririko wa shehena mbalimbali za mizigo zilizohudumiwa kwa mujibu wa utaratibu.

“Mwaka 2014/15, tumehudumia tani 100,000, 2015/16, tumehudumia 139,000 kulikuwa na ukuaji wa asilimia 28,   2016/17 ukahudumia tani chini kidogo ya mwaka 2015/16, tani 137,000 kwa hiyo tulishuka kwa asilimia 1.14

“Lakini 2017/18.tulihudumia tani 196,0000  kwa hiyo ukuaji wake pale ulikwenda kwa kasi zaidi wa asilimia 30.02 na mwaka uliofuata mwaka jana wa 2018/19 umehudumia tani 199,831 sawasawa na ukuaji wa asilimia 1.14 ukilinganisha na mwaka 2017/18 kwa hiyo hapa utaona kuna ukuaji na hsa kwenye kipindi hiki cha Serikali ya Awamu ya Tano kuanzia ile 2016/17 mpaka kwenye 2018/19,” alisema

Alisema kwa mwaka wa fedha 2019/20,bandari hizo, zimejiwekea lengo la kuhudumia tani 210,000 sawa na ongezeko la asilimia 9, ukilinganisha na mwaka jana na kwenye mapato vilevile kwa sababu shehena unayohudumia ndio vilevile pia na ukuaji wa wa mapato.

“Mwaka 2014/15 tulikuwa na bilioni 2. 09 ya mapato, mwaka 2015/16 bilioni 2.667, mwaka 2016/17  bilioni 4. 14 kwa hiyo utaona kuna ukuaji wa mapato.

“2017/18 hapa tulipiga zaidi tulikwenda mapato ya bilioni 5. 93 na mwaka uliofuata mwaka jana tumekwenda na mapato ya bilioni 4. 148 ambapo hiyo tulishuka kidogo na sababu kubwa tilirekebisha tozo,” alisema Meneja huyo

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,590FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles