27.5 C
Dar es Salaam
Friday, July 1, 2022

TPA yawatoa hofu wafanyabiashara DRC

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko.
Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

MAMLAKA ya Bandari nchini (TPA), imewahakikishia wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi usalama wa mizigo yao katika Bandari ya Dar es Salaam.

Aidha, mamlaka hiyo imesema ulinzi umeimarika na kwamba suala la wizi  katika bandari hiyo kwa sasa ni historia.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko, aliyasema hayo hivi karibuni alipokutana na wafanyabiashara wakubwa katika miji ya Bukavu na Goma katika Jimbo la Kivu Kusini na Kaskazini lililopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Alisema hali ya usalama katika njia ya kati itaimarishwa kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kudhibiti masuala ya uhalifu yanayotokea njiani, hali inayowakatisha tamaa wasafirishaji wa bidhaa zenye thamani kubwa kama madini na vitenge.

Pamoja na mambo mengine, Kakoko alisema Serikali imejipanga kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara ili kuleta ufanisi katika  biashara zao.

“Serikali ya Tanzania imedhamiria kujenga reli mpya ya kisasa na ya kiwango cha kimataifa itakayorahisisha usafirishaji katika njia ya kati pamoja na kujenga miundombinu ya kisasa katika Bandari Kavu ya Isaka.

“Hii itasaidia wafanyabiashara wa DRC kutolazimika kwenda umbali mrefu hadi Dar es Salaam kufuatilia mizigo yao, badala yake itatumika bandari kavu ya Isaka itakayokuwa pamoja na mambo mengine njia ya reli na kituo cha forodha,” alisema.

Kakoko alisema kwa sasa Serikali inatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo yenye lengo la kuboresha huduma ndani ya bandari, ikiwa ni pamoja na kufanya kazi saa 24 kila siku ili kuwapunguzia adha wafanyabiashara.

Alisema hatua hiyo itasaidia kupunguza muda wa kutoa mizigo ndani ya bandari ambapo endapo mfanyabiashara atakuwa amekamilisha malipo yote ya forodha, ataweza kuutoa mzigo huo katika muda usiozidi saa 48.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
195,419FollowersFollow
544,000SubscribersSubscribe

Latest Articles