22 C
Dar es Salaam
Sunday, May 28, 2023

Contact us: [email protected]

TPA YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA LINDI

Na Hadija Omary, Lindi

Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Kanda ya Mtwara imezipatia vifaa tiba vyenye thamani ya Sh milioni 33.3 halmashauri mbili za mkoa wa Lindi kwa lengo la kuboresha huduma mbalimbali za afya kwa wananchi wake.

Vifaa hivyo ni pamoja na vitanda vinane kwa ajili ya kujifungulia na darubini sita zikazofanya kazi za kiuchunguzi wa kimaabara katika vituo mbalimbali vya afya.

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa uongozi wa halmashauri hizo, Meneja wa Bandari mkoani Mtwara Nelson Mlali amesema lengo la kutoa msaada huo ni kuboresha huduma za Afya kwa wananchi.

“Sisi tunaanza tu, lakini wenzetu wengi wanatusikia, nina imani watajitokeza kutuunga mkono ili kutatua changamoto hizi za afya kwani ni wazi kwamba changamoto za sekta ya afya ni nyingi na hatutaweza kuzimaliza kwa siku moja au kumaliza kwa kujitolea kwa taasisi nyingine hivyo natoa wito kwa taasisi nyingine kuunga mkono jitihada hizi,” amesema Mlali.

Meya wa Manispaa ya Lindi, Mohamed Lihumbo ameishukuru mamlaka hiyo kuwa msaada huo na kuongeza kuwa umefika kipindi muafaka wakati ujenzi wa vituo vipya vya afya ukiendelea kwenye kata mbalimbali.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Dk. Ally Zuberi na Mganga Kituo cha Afya cha Mjini cha Manispaa Lindi, Richard Juma wamesema upatikanaji wa vifaa hivyo utawasaidia kutekeleza majukumu ya utoaji bora wa huduma kwa wagonjwa wanaofika kupata tiba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,169FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles