28.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

TPA yatoa msaada wa mashine za kuhifadhi watoto njiti Tanga

Amina Omari,Tanga

Mamlaka ya usimamizi wa bandari Tanzania (TPA), imetoa msaada wa mashine mbili za incubator kwaajili ya kusaidia kuhifadhi watoto njiti zenye thamani ya Sh milioni 25 katika Hospitali ya rufaa ya Bombo mkoani Tanga.

Akikabidhi msaada huo Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mhandisi Witonde Philipo, amesema kuwa mamlaka hiyo ilikuwa imetenga bajeti ya Sh milioni 50 kwa ajili ya kusaidia jamii katika sekta ya elimu na afya.

Mashine mbili za kusaidia kuhifadhi watoto njiti

Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa mkoa huo, Abdiel Makange, amesema mashine hizo zitaweza kusaidia kuokoa maisha ya watoto njiti ambao wanazaliwa katika hospitali hiyo.

“Hospitali ilikuwa ina mashine mbili tayari, hivyo uwepo wa nyingine za ziada kutawezesha kupunguza changamoto ya vifo kwa watoto hao” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles