MWANDISHI WETU-MWANZA
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imesema kuwa inakabiliana na changamoto ya uwepo wa bandari bubu zaidi ya 300 katika Ziwa Victoria.
Imesema kuwa kwa sasa wanapambana kwa mujibu wa sheria ili ziweze kuondoka kwa kuzirasimisha ili ziweze kutambulika jambo ambalo litasaidia kuleta ufanisi katika ukusanyaji wa mapato ya Serikali huku akitenga zaidi ya Sh bilioni 16 kwa ajili ya kuboresha na kujenga bandari zilizopo katika ziwa hilo.
Bandari hiyo kwa sasa imeanza kuhudumia kwa kusafirisha mizigo katika nchini za Uganda, Sudani Kusini na Rwanda.
Kauli hiyo imetolewa leo na Meneja wa Bandari za Ziwa Victoria, Morris Machindiuza, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shughuli za bandari zilizopo ndani ya ziwa hilo.
Amesema pamoja na hilo TPA imepewa jukumu ya kuendeleza bandari na kuendesha, kutangaza huduma za bandari kwa kushirikiana na sekra binafsi katika uendeshaji wa bandari.
“Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania katika Ziwa Victoria imejipanga na tayari ilikishaanza kuhudumia shehena mbalimbali kama vile za Shirika la Chakula Duania (WFP), mashudu, viwanywaji baridi pamoja na kusafirisha vifaa vya ujenzi kwa ajili ya nchi za Uganda na Sudani Kusini.
“Katika mwambao wa Ziwa Victoria TPA inamiliki na kusimamia bandari kubwa za Mwanza Kaskazini na Kusini, Nansio, Kemondo Bay, Bukoba na Musoma pia kuna bandari zingine ndogo za mwambao zaidi ya 15 ambazo zote tunazihudumia kwa kuwa chini ya usimamizi wetu,” amesema Machindiuza
Pamoja na hilo amesema kuwa TPA inaendesha Bandari Kavu ya Isaka ambayo inamilikiwa na Shirika la Reli Tanzania ambapo kuwa ghala kubwa lenye uwezo wa kuhifadhi shehena ya tani 3,000, yadi ya makasha na yadi ya Rwanda yenye eneo la ekari 17.05.
Meneja huyo wa Bandari za Ziwa Victoria, amesema kuwa kwa sasa wapo mbioni kuanzisha Bandari Kavu nyingine ya Fela wilayani Misungwi mkoani Mwanza ambapo hadi sasa tayari wamelipa fidia kwa nyumba 14 na mpango wa matumizi ya ardhi unaandaliwa katika eneo eno hilo.
Amesema kwa kipindi cha mwaka 2014/15 hali ya utendaji kwa Bandari za Ziwa Victoria ulidorora kwa muda kutokana na kushuka kwa hali ya utendaji wa Reli ya Kati na kupungua kwa idadi ya meli zinazofanya kazi katika Ziwa Victoria.
“kwa miaka mitano iliyopita 2014/2015-2018/2019 shehena inayohudumiwa katika Bandari ya Mwanza imekuwa ikipanda kwa wastani wa asilimia 0.5 kwa kutoka tani 129,767 mwaka 2014/15 hadi tani 157,808 mwaka 2018/19.
“katika kipindi cha miezi minne ya kwanza mwaka 2019/20 Julai hadi Novemba Bandari ya Ziwa Victoria imeweza kuhudumia tano 76,168.44 ikiwa ni asilimia 99.14 ya lengo la kuhudumia tani 76,833,” amesema Machindiuza
Akizungumza hali ya mapato amesema imepanda kutoka Sh milioni 600 hadi kufikia Sh bilioni 1.4 jambo ambalo ni la kutia moyo katika uendeshaji wa shughuli za bandari.
“Kwa sasa Serikali ya Awamu ya Tano mkakati mkubwa ni kukusanya mapato ya ndani, nasi TPA kama wadaui taasisi muhimu tunalizingatia hilo kwa kuhakikisha tunatafuta wafanyabishara ambao ilin waweze kutumia bandari zetu,” amesema Machindiuza