22 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

TPA: Lango ya uchumi lipo Ziwa Tanganyika

MWANDISHI WETU-KIGOMA

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), imesema kuwa lango la uchumi nchini lipo Ziwa Tanganyika kutokana na ziwa hilo kupakana na nchi tatu zenye tapo la utajiri Afrika.

Kutokana na hali hiyo imesema kuwa thamani ya madini yaliyopo Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) unaofikia dola za Marekani trilioni 24, zinahitaji usafirishaji wa uhakika kufika katika soko la dunia.

Meneja wa Bandari za Ziwa Tanganyika, Percival Salama ametoa kauli hiyo leo mjini Kigoma alipokua akizungumza na waandishi wa habari waliopo kwenye ziara ya kutembelea miradi inayotekelezwa na TPA katika maziwa makuu nchini.

Amesema Bandari za Ziwa Tanganyika zipo katika mikoa mitatu ya Kigoma, Katavi na Rukwa kwa upande wa Tanzania ambapo pia ziwa hilo limepakana na nchi nne kwa pamoja ambazo ni Tanzania yenyewe, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Zambia pamoja na Burundi.

“Na kama unatafuta asilimia ya kila nchi kwenye Ziwa Tanganyika Tanzania ina asilimia 45, DRC 41, Burundi asilimia 8 na Zambia asilimia 6. Na Ziwa Tanganyika ndilo Ziwa la pili kwa kina kirefu duniani lina wastani wa urefu wa kina cha mita 1470, kwa hiyo ukizungumzia uimara wa Biashara ya kuhudumia nchi hizi nne maana yake unazungumzia miaka mingi ijayo.

Shehena ya mizigo ikiwa katika Bandari ya Kigoma kwa ajili ya kusafirishwa katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Burundi

“Kwa hiyo ni sahihi na ni vyema kabisa kwa serikali za nchi hizi nne zinapofanya uwekezaji wa miundombinu ya Bandari pamoja na vyombo vya usafirishaji ili kuhakikisha kwamba wananchi wa nchi hizo wanapata huduma.

“Lakini la pili ambalo nataka niliguse kwenye hili eneo ni kwamba Ziwa Tanganyika na mikoa inayopakana na Ziwa Tanganyika na nchi hizi tumelala kwenye utajiri wa kutupwa yaani tupo sisi Tanzania kwenye ukanda wenye utajiri wa kutupwa duniani sio tu katika Afrika.

“Unazungumzia Tanzania kama nchi tajiri kama anavyosema Mheshimiwa Rais Magufuli mara nyingi na wote sasa Watanzania tunajua kwamba Tanzania ni tajiri na kilichobaki ni fikra kuitumia vizuri ili kutumia vizuri fursa ile ya utajiri tulikuwa nao kubadilisha maisha ya nchi yetu kiuchumi pamoja na wananchi wake,” amesema Salama.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,504FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles