23.2 C
Dar es Salaam
Friday, June 9, 2023

Contact us: [email protected]

TP Mazembe: Ukuta Yanga ni imara

V.Bossou
V.Bossou

NA ADAM MKWEPU, DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Hubert Velud, amesema uimara wa safu ya ulinzi ya Yanga uliwapa wakati mgumu wa kufunga mabao kutokana na washambuliaji wake kushindwa kupita kwenye ukuta huo.

Timu hizo zilikutana juzi katika mchezo wa pili wa Kundi A wa Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo wenyeji Yanga waliambulia kipigo cha bao 1-0.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Velud ambaye ni raia wa Ufaransa, alisema licha ya kuwafunga wapinzani wao ugenini washambuliaji wake walipata tabu kuichambua ngome imara ya Yanga hivyo kulazimika kutumia mbinu ya kupiga mipira mirefu.

Alisema mshambuliaji wa Tanzania, Thomas Ulimwengu, anayekipiga kwenye kikosi hicho, ndiye alikuwa nyota wa mchezo kwa upande wa kikosi, kwani ubora wake ulichangia kupatikana kwa bao pekee la ushindi lililofungwa dakika ya 73 kufuatia mpira wa adhabu uliopigwa baada ya kuangushwa nje kidogo ya eneo la hatari.

Katika mchezo wa juzi safu ya ulinzi ya Yanga iliongozwa na mabeki; Kelvin Yondani, Vicent Bossou, Mbuyu Twite na Juma Abdul.

Kwa upande wake Kocha Mkuu wa Yanga Mholanzi, Hans van der Pluijm, alisema uzoefu wa mechi za kimataifa na uimara wa wapinzani wao TP Mazembe ndio  ulichangia timu yake kushindwa kuibuka na ushindi juzi licha ya wachezaji kuonyesha kiwango cha juu.

Alisema pamoja na kikosi cha TP Mazembe kupata uzoefu wa kutosha katika mechi za kimataifa, pia wachezaji wake wana nguvu ya kupambana na timu pinzani.

“Kipindi cha kwanza wachezaji walipambana kadiri ya uwezo wao na kuonyesha kiwango cha uhakika lakini walishindwa kutumia vyema nafasi walizotengeneza za kufunga.

“Ubora wa kikosi cha TP Mazembe ulitufanya tuzidiwe eneo la kiungo baada ya wachezaji wanaocheza nafasi hiyo kupoteza hamasa ya kupambana kipindi cha pili ambacho walipata bao la ushindi,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,351FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles