31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

TOZO ZA KUMWONA DAKTARI KUFUTWA

Na Amina Omari-Tanga


SERIKALI imesema inaangalia uwezekano wa kufuta tozo ya kumwona daktari kwa wagonjwa wanaotakiwa kufanyiwa uchunguzi wa awali wa saratani.

Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, wakati wa uzinduzi wa chanjo pamoja na uchunguzi wa saratani ya mlango wa kizazi mkoani Tanga.

Alisema kama Serikali inafadhili matibabu ya ugonjwa huo, wataangalia uwezekano wa kutoa malipo ya kumwona daktari ili wananchi waweze kupata fursa ya matibabu vizuri zaidi.

“Hili la malipo ya kumwona daktari ni la kuliangalia kwa mapana hasa kwa wale wanaokwenda kuangalia saratani ili kumpunguzia mwananchi wa hali ya chini gharama,” alisema Ummy.

Kwa upande wa chanjo ya saratani kwa wasichana wenye umri wa miaka 14, alisema wamejipanga kuhakikisha wanawafikia wasichana zaidi ya 600,000 nchi nzima.

Waziri huyo aliiagiza mikoa kuhakikisha wanahamasisha wazazi ili kufikia lengo la kuwapatia chanjo wasichana wote wenye umri wa miaka 14 waweze kujikinga na saratani ya mlango wa kizazi.

Naye Mratibu wa Chanjo Mkoa wa Tanga, Seif Shaib, alisema lengo walilojiwekea ni kuhakikisha wanawafikia wasichana 38,000.

Alisema kwa sasa wameanza kutoa elimu ya uhamasishaji kwa wazazi ili kuwa na uelewa na kuwaruhusu mabinti zao kupatiwa chanjo hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles