22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 28, 2021

Tonton Fwamba kuileta ‘Chofele’

KENTUCKY, MAREKANI

MWANAMUZIKI wa miondoko ya Rhumba anayeishi Kentucky nchini Marekani, Tonton Fwamba, amesema mashabiki zake wakae tayari kupokea video ya wimbo, Chofele.

Akizungumza na MTANZANIA, Fwamba aliyewahi kutamba na wimbo, Zua Lokumu na My Fito alisema amekuwa akipokea jumbe nyingi kutoka kwa mashabiki wakitaka video ya wimbo huo uliotoka Februari mwaka huu.

“Audio ilipokewa vizuri, sasa najiandaa kutoa video kwahiyo mashabiki wakae karibu na chaneli yangu ya YouTube ili nikiachia waweze kuipata,” alisema mwanamuziki huyo mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
158,502FollowersFollow
519,000SubscribersSubscribe

Latest Articles