27 C
Dar es Salaam
Friday, May 27, 2022

Toni Braxton amkataa Rodman

 NEW YORK, MAREKANI 

MKALI wa muziki na filamu nchini Marekani, Toni Braxton, amekanusha taarifa kwamba, aliwahi kuwa kwenye uhusiano na nyota wa mchezo wa kikapu nchini humo Dennis Rodman. 

Rodman ambaye aliwahi kutamba na timu mbalimbali za kikapu kama vile Los Angeles Lakers, Chicago Bulls na zingine nyingi, alitajwa kuwa mmoja kati ya nyota wa mchezo huo ambao walitoka na warembo wenye majina makubwa nchini humo kama vile Madonna, Carmen Electra, Vivica Fox, na Toni Braxton. 

Lakini Toni amekanusha taarifa hiyo na kudai walikuwa kama marafiki na hakuna kitu chochote ambacho kiliendelea kama watu wanavyodhani. “Sikuwahi kutoka kimapenzi na Dennis Rodman, alikuwa kama rafiki yangu kwa kuwa mara ya kwanza tulikutana kwenye tuzo za MTV mwaka 1996,” alisema Toni. Aliongeza kwa kudai kwa sasa yupo kwenye mipango ya kufunga ndoa na mpenzi wake ambaye ni bosi wa kundi la Cash Money, Birdman, baada ya kuwa pamoja tangu 2018. 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
192,454FollowersFollow
541,000SubscribersSubscribe

Latest Articles