26.1 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

TOKA KALAPINA HADI TID: ITAPENDEZA MKIFANYA KOLABO KUHARAMISHA UNGA

Hakuna asiyefahamu kinachoongelewa kwa sasa hapa nchini kuhusiana na kadhia ya uraibu wa dawa za kulevya unaomaliza nguvu kazi ya taifa hili, hususan rasilimali watu kupitia vijana ambao wanadhoofisha maisha yao na kuwatajirisha wasambazaji na wauzaji wa dawa hizo, ambazo ni mwiba duniani, si tu huku kwetu hata nchi walizoendelea ambapo zimeangamiza maisha ya ‘mastaa’ mbalimbali.

Najua wachache nikiwauliza kama mnamfahamu ‘Staa’ yoyote wa kimataifa aliyeangamizwa na kadhia hiyo mtanitajia Whitney Houston lakini kwa kuwa muziki wa Rock hauna mashabiki wengi hapa Bongo kwenye mtindo huo ndipo wameangamia wengi zaidi tena katika siku za hivi karibuni, ambao kazi zao zilizofanyiwa matoleo mbadala (remix) ziligubika mashabiki wengi duniani.

Bongo iko duniani kwa hiyo nayo haikusalimika katika wimbi hilo na mastaa wetu tuliowaona wakisotea mafanikio kwa taabu hadi kukwea kwenye umaarufu, wametepeta na kupotezwa kwenye gemu huku maisha yao yakiwa hatarini kutokana na kudhoofika kwa afya zao, inasikitisha!

Lakini ‘Back’ hiyo inaelekea kumalizika ikiwa umakini utawekwa katika mapambano yaliyopata msukumo mpya, kutoka kwa kijana wa upande mwingine ambaye si mwanamuziki wala msanii lakini ni mtendaji wa serikali akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam aliyeguswa na kuangamia kwa vijana wenzake akaamua kuwa wa kwanza kumshika fahali kwenye mapembe na kusababisha wengine waliokuwa na hofu ya kuvaa madaluga na kujitosa kwenye mtanange huo dhidi ya ‘unga’ nao wapate ujasiri wa kusimama kifua mbele na kudiriki kuongoza mapambano.

‘Front’ yetu kwa vita hii itagubikwa na majina mengi lakini katika askari wapambanaji licha ya Paul Makonda, nitaongezea majina mengine mawili nikianza na mwana ‘Kemo’ (Hip-Hop) mbobevu Kalapina kutoka Block 41 na Mnyama aliyepotea njia ambaye sasa anarudi kwenye mashiko yake, Khalid Mohamed a.k.a TID, nina sababu ya kuweka majina hayo matatu licha ya kuwepo mengi yanayoweza kuorodheshwa.

Makonda nimeshamuelezea lakini Kalapina nampa saluti kubwa ingawa wakati huo ni kama Wabongo hawakumwelewa lakini alijigeuza jeshi la mtu mmoja na kupitia ‘crew’ yake ya Kikosi Cha Mizinga waliendesha kampeni ya: ‘Hip-Hop bila madawa ya kulevya inawezekana’ lakini ‘Back’ hiyo ni kama hakusomeka kumbe alichokisema wakati ule ndiyo kinajidhihirisha sasa na tunaweza kutohoa mara mbili usemi wake: ‘Bongo-Fleva bila madawa ya kulevya inawezekana’ kama alivyosema TID lakini pia tukihausha tena inakuwa hivi: ‘Tasnia ya sanaa bila madawa ya kulevya inawezekana’.

Hapo ndipo utakapompigia saluti Kalapina manake alivaa unabii kwa kusema ambacho sasa ndiyo habari iliyoko midomoni mwa Wabongo wote, kwa Mnyama TID ‘attitude’ yake inavutia manake hakuweka kinyongo na ameonesha kuwa alikosea na hata kujitokeza hadharani kukiri na kuahidi kujirekebisha pia kusaidia katika mapambano, kudos kwako Mnyama!

Lakini kuna mawili tunayoweza ‘kuya-front’ katika vita hii, vipi kama TID na Kalapina mkija na Kolabo ya kupinga ‘unga’ au wanamuziki idadi kadhaa wakiibuka na songi la pamoja kama ilivyokuwa ‘We Are The Wold’ kuhamasisha vita hii inayotukabili? Tuinuke, twende tukapambane, ushindi upo!

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles