24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Tofauti kati ya ndege za Boeing, AirBus

airbusboeing-86771

NA FARAJA MASINDE

TEKNOLOJIA ya ndege inazidi kukua kila kukicha, huku kampuni mbili za kutengeneza ndege za Boeing na AirBus zikionekana kuchuana zaidi. Leo hebu tuangalie tofauti zilizopo kati ya ndege hizi mbili.

Kabla hatujazungumzia tofauti kubwa iliyopo baina ya Airbus na Boeing ambazo ni kampuni kubwa zinazotengeneza ndege za biashara duniani, kwanza lazima ufahamu kuwa Boeing ndio kinara, hii inatokana na ukubwa wake pamoja na kuwa na umbo kubwa.

Hata hivyo, ni lazima utambue kuwa Airbus nayo bado ina nafasi kubwa, hii inatokana na mauzo mazuri ya ndege zake kwa kipindi cha mwaka 2013.

Takwimu zinaonyesha kuwa 2013, Airbus iliongoza kwa mauzo ikiwa imeuza ndege 1,503 huku Boeing ikiuza ndege 1,355 pekee.

Hata hivyo, Airbus ilikusanya mapato bilioni 13 kiwango ambacho ni cha chini ukilinganisha na kilichokusanywa na Boeing kwa mwaka huo.

Tofauti iliyopo ni kwamba, Airbus zinatengenezwa nchini Ufaransa huku zikitumia malighafi kutoka Ujerumani, Hispania na Uingereza.

Awali, ilianza kama muungano wa wazalishaji lakini baadaye walijiimarisha na kupewa kibali cha kufanya biashara hiyo.

Kwa sasa kampuni hiyo inazalisha ndege kubwa za abiria duniani za A380 ambazo zimeonekana kuwa tishio kwa wapinzani wao sokoni, ambao ni Boeing hasa baada ya kuanza biashara mwaka 2007.

Hata hivyo, sababu nyingine inayozibeba ndege za Airbus ni kutokana na kuwa mpya na za kisasa zaidi huku zikitajwa kuwa na ufanisi, hasa kuanzia ile ya A 350.

Hii inatajwa kuwa na ubunifu zaidi katika utengenezaji katika umbo lake ikilinganishwa na Boeing 787.

Hili ni Shirika la Marekani kwenye eneo la Chikago, ambalo lilianzishwa kwa mazingira yale yale yaliyotumika kuanzisha Airbus, lengo lilikiwa ni kushindana na kampuni ya McDonnel Douglas mwaka 1977.

Boeing waliingia sokoni na ndege yao ya 787 Dreamliner.

Ndege hii ilisaidia kuongeza ufanisi wa mafuta na kupunguza athari za mazingira.

Kwa mara ya kwanza ilipata matatizo mwaka 2007 ambapo hata hivyo, Boeing iliingiza sokoni ndege mpya aina ya 787 ambayo imesaidi kampuni hiyo kuchuana na mshindani wake Airbus.

Maoni 0653045474.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles