26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, October 27, 2021

TOENI UMUHIMU KUHUSU HAKI ZA BINADAMU

Na CLARA MATIMO-MWANZA

KAMISHNA wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), Salma Ali Hassan, amewataka waandishi wa habari nchini kuandika na kuripoti kwa umma kuhusu taarifa za matukio ya matumizi mabaya ya madaraka, ukiukwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora bila ubaguzi wala upendeleo.

Akifungua warsha ya siku moja iliyoandaliwa na THBUB Kanda ya Ziwa na kukutanisha waandishi wa habari 39 kutoka vyombo mbalimbali vya habari ili kuwajengea uwezo katika kuripoti na kufikisha  taarifa za matukio tofauti tofauti kwa umma yenye  mtazamo wa haki za binadamu jijini Mwanza juzi, Salma alisema matukio hayo yamekuwa yakiongezeka hapa nchini.

Alisema matukio hayo ni pamoja na mauaji ya vikongwe kwa imani ya ushirikina na kufukuliwa makaburi ya watu wenye ualbino, hivyo ni wajibu wa waandishi wa habari kuandika habari hizo ili kuihamasisha Serikali, asasi zisizo za serikali na wadau wengine wa masuala ya haki za binadamu ili  kuleta mabadiliko ambayo yataboresha maisha ya watu.

 “Vyombo vya habari na waandishi wa habari  ni walinzi na watetezi muhimu wa haki za binadamu, ninyi ni macho, masikio na sauti ya umma, mara nyingi mnaweka wazi masahibu yaliyowapata watu kwenye mazingira yaliyo nje ya uwezo wao, aidha kwa kudhalilishwa au kuonewa na watu wengine.

“Hapa ndipo kiini cha mafunzo ya leo, THBUB tunatarajia baada ya mafunzo haya waandishi wa habari wote mlioshiriki leo mtaona umuhimu wa hali ya juu na umakini usiotiliwa shaka kuandika na kuripoti taarifa za masahibu hayo kwa umma kwa mtazamo wa haki za binadamu,” alisema Salma.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
163,388FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles