26.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 2, 2023

Contact us: [email protected]

TNMC yawataka wauguzi kusimamia viapo vyao

Na Ramadhan Hassan,Dodoma

Jumla ya Wauguzi na Wakunga 1,949 wamepatiwa leseni na vyeti vya usajili na Baraza la Uuguzi na Ukunga Tanzania (TNMC) huku Mwenyekiti wa Baraza hilo, Profesa Lilian Mselle akiwataka kusimamia viapo walivyoviapa.

Leseni na vyeti hivyo wamevipata mara baada ya kufaulu mitihani iliyotolewa na Baraza la Ukunga na Uuguzi Tanzania (TNMC)

Akizungumza Machi 18, 2023 wakati wa mahafali hayo yaliyofanyika jijini Dodoma hapa, Prof. Mselle amesema wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii kwani kada yao ni muhimu na Taifa linawategemea.

“Nendeni kashughulikieni, magonjwa ya milipuko,vifo vya kina mama na magonjwa ambayo siyo ya kuambukiza, fanyeni kazi kwa nguvu wagonjwa wafurahi katekelezeni kiapo mlichokiapa,”alisema Prof. Mselle

Kwa upande wake Mkunga, Emmanuel Ngaila amesema watafanya kazi kwa bidii kwa kuzingatia viapo walivyoapa.

“Tutahakikisha kile tulichokisomea na tulichojifunza kwa vitendo tunakifanyia kazi,”amesema Ngaila.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa usajili, leseni na maadili kutoka Baraza la Ukunga na Uuguzi, Jane Mazigo amewataka wakunga na wauguzi kutochukua rushwa, kuangalia maslahi ya wagonjwa,wawe waadilifu na wasitoe siri za wagonjwa.

“Choma sindano vizuri,msijiingize kwenye vikundi vibaya,msiwaze ubosi huo unakuja wenyewe kwa kufanya kazi,tunza heshima yako, toa huduma kwa upendo, kuweni wasafi na itumieni vizuri mitandao ya kijamii,” amesema Mazigo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,405FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles