21 C
Dar es Salaam
Friday, August 12, 2022

TNBC kutumia bilioni 1/- mapinduzi ya kiuchumi

Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM

BARAZA la Taifa la Biashara (TNBC) limesema kuwa katika kutekeleza mpango kazi wake nusu ya mwaka wa fedha wa 2019/2020 na kuchangia vikubwa mapinduzi ya kiuchumi Tanzania, linatarajia kutumia Sh 1,104,590,000.

Katika taarifa iliyotolewa Dar es Salaam kuhusu shughuli za baraza kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2019/20, baraza hilo licha kutoa mchanganuo wa mkiasi cha fedha utakaochangwa na wadau, lakini limesema litapokea mgawo wa Serikali, mgawo wa mradi wa LISC na mgawo kutoka wadau wengine.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba TNBC inatazamiwa kuchangia vikubwa katika mapinduzi ya kiuchumi Tanzania.

Pamoja na mambo mengine, baraza linatarajia kushirikiana na Tamisemi kuhakikisha mabaraza ya mikoa na wilaya yanakutana kama ilivyoainishwa kwenye mwongozo.

“Itafanyika jitihada ya kuimarisha baraza na kuwa kitovu cha taarifa zinazohusu maboresho ya mazingira ya biashara nchini na kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kufanya tafiti zitakazochochea majadiliano yenye tija kati ya sekta ya umma na sekta binafsi.

“Katika hili, baraza linatarajia kufanya majadiliano katika maeneo kama ushiriki wa mwanamke katika uwekezaji na biashara, ikiwemo changamoto zake, changamoto zinazokabili biashara ndogo ndogo na za kati na fursa zilizopo,” ilieleza taarifa hiyo.

Baraza pia litaendelea kuimarisha ushirikiano uliopo kati ya sekta binafsi na sekta ya umma katika kuchochea mapinduzi ya kiuchumi nchini.

“Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Mheshimiwa Rais John Magufuli, imewekeza kwa kiasi kukubwa katika sekta ya usafirishaji.

“Hivyo basi ni muhimu kwa baraza kuonyesha fursa mbalimbali zilizopo kwenye sekta ya usafirishaji na jinsi Watanzania wanavyoweza kujikomboa kiuchumi kupitia kwenye mnyororo wa thamani wa sekta ya usafirishaji,” ilisema taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,507FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles