28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

TMDA yateketeza tani 35,647 za dawa zisizofaa

Ramadhan Hassan, Dodoma

Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) katika kipindi cha 2021/22 imeteketeza tani 35,547 za dawa zisizofaa kwa matumizi ya binadamu.

Kiasi hicho kama kingepelekwa sokoni kilikuwa na thamani ya zaidi ya Sh35 bilioni na kwamba kingeweza kuleta madhara kwa watu wengi.

Kauli hiyo imetolewa Julai 29,2022 na Mkurugenzi wa TMDA, Adam Fimbo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu taarifa ya utekelezaji wa shughuli zao kwa mwaka 2021/22.

Fimbo pia amesema TMDA imebaini kemikali 93 kuwa kwenye bidhaa ya tumbaku jambo linaofanya zao hilo kuendelea kuwa katika mtihani mgumu sokoni lakini Serikali haiwezi kuzuia kwa kuwa linatumika kwa shughuli za biashara pia.

Kwa mujibu wa Fimbo, pamoja kiasi hicho kikubwa kutekelezwa, lakini hawana mtu wanayemshikiria au kiwanda cha dawa kilichozuiwa kwani kazi yao ni kuendelea kutoa elimu na kwa baadhi ya watu ni kuwapiga faini.

Mkurugenzi huyo ametangaza kuongeza kasi kwa ajili ya kudhibiti dawa zisizofaa zisiingizwe sokoni na kwa matumizi ya watu ili kuendelea kulinda afya za Watanzania ambalo ni jukumu lao.

Amesema jumla ya dawa na vifaa tiba 8,831 vimesajiliwa nchini hati kufikia sasa ambapo viwanda 17 vya dawa vimeruhusiwa na 17 ni vinavyotengeneza vifaa tiba huku 26 vikiwa ni viwanda vifaa tiba na 6 ni viwanda wa gesi tiba.

“Tunavyo jumla ya vituo vya forodha 32 ambavyo kwa baadhi ya maeneo vinafanya kazi saa 24 hasa katika Jiji la Dar e salaam, lengo letu ni kuendelea kuwa Mamlaka bora yenye udhibiti wa kusaidia jamii ya Watanzania,” amesema Fimbo.

Kingine ametaja maeneo 10,938 yanayojihusisha na biashara ya dawa,chanjo,vifaa tiba na vitendanishi yalikaguliwa katika kipindi hicho ikilinganishwa na maeneo 10,846 yaliyokaguliwa mwaka 2020/21.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles