23.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

TMA yatoa tahadhari mafuriko yaja

Bethsheba Wambura, Dar es Salaam

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) imetoa tahadhari ya kuwepo kwa mvua kubwa zitakazosababisha mafuriko katika baadhi ya mikoa nchini kwa muda wa siku tano.

Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo Jumanne Desemba 18, imeitaja mikoa ambayo leo itakuwa na mvua kubwa ni Njombe, Ruvuma na Morogoro Kusini na kesho Jumatano Desemba 19 maeneo yanayotarajiwa kuwa na mvua ni Rukwa, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa, Ruvuma, Dodoma, Singida, Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Tanga, Pwani, Dar es Salaam, Lindi, Mtwara, Ruvuma,Morogoro, Unguja na Pemba.

“Kuanzia Jumatatu Desemba 17 hadi Ijumaa Desemba21 kutakuwa na mvua kubwa ambazo zitasababisha maji kujaa na kupita kwa kasi jambo ambalo ni hatari kwa maisha ya watu.

“Hivyo, mamlaka inatoa tahadhari kuwa mvua hiyo itakayoambatana na upepo na kusababisha msongamano wa magari na watu na hivyo kuchelewesha usafirishaji hasa katika maeneo ya mijini hivyo watu wa maeneo hayo wanapaswa kuchukua tahadhari zitakazoachwa na mvua hiyo mapema,” imesema taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles