26.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, December 11, 2024

Contact us: [email protected]

TMA yatahadharisha mvua Mikoa ya Pwani

Na Brighiter Masaki, Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania (TMA) na (Kaimu Mkurugenzi Mkuu), Dk. Hamza Kabelwa, ametangaza taarifa ya utabiri wa hali ya hewa kwa msimu wa mvua za Masika ambao ni mahususi kwa maeneo ya nyanda za juu Kaskazini Mashariki.

Amesema Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro, Pwani ya Kaskazini (Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Mikoa ya Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba).

Maeneo mengine ni ukanda wa Ziwa Victoria (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara) pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma.

Dk. Kabelwa amesema kutokana na mifumo ya hali ya hewa ilivyo kwa sasa na inavyotarajiwa katika kipindi chote cha msimu (kama ilivyoelezwa katika kipengele cha III cha taarifa hii), kwa ujumla mvua za wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi ya nchi yanayopata misimu miwili ya mvua kwa mwaka.

“Hata hivyo, maeneo mengi ya nyanda za juu kaskazini mashariki na ukanda wa ziwa Viktoria yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani.

“Aidha, maeneo ya Pwani ya Kaskazini yanatarajiwa kupata mvua za wastani hadi chini ya wastani. Msimu wa mvua za Masika unatarajiwa kuambatana na vipindi vya mvua kubwa hususan katika kipindi cha mwezi Machi,” amesema Dk. Kabelwa.

Taarifa hiyo inasema katika ukanda wa Ziwa Viktoria: (Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma (wilaya za Kakonko na Kibondo)

Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya ukanda wa Ziwa Victoria pamoja na kaskazini mwa mkoa wa Kigoma. Mvua hizi zinatarajiwa kuanza katika wiki ya kwanza ya mwezi Machi, 2021 na kuisha katika wiki ya nne ya mwezi Mei, 2021.

Ukanda wa Pwani ya Kaskazini: (kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, mikoa ya Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Dar es Salaam, Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba):

“Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi chini ya wastani katika maeneo mengi ya ukanda wa pwani ya kaskazini. Mvua katika maeneo haya zinatarajiwa kuanza mapema katika wiki ya nne ya mwezi Februari, 2021 na zinatarajiwa kuisha katika wiki ya tatu ya mwezi Mei, 2021.

Amesema Kwa upande wa Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki Mikoa ya Arusha, Manyara na Kilimanjaro) Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi na zinatarajiwa kuanza mapema katika wiki ya nne ya mwezi Februari, 2021 na kuisha katika wiki ya tatu ya mwezi Mei, 2021.

Pia Katika kipindi cha Masika (Machi hadi Mei, 2021) hali ya unyevunyevu wa udongo na maji ya kutosha kwa ajili ya umwagiliaji inatarajiwa.

“Hata hivyo, hali hiyo ya unyevunyevu hususan katika maeneo ya ukanda wa ziwa Victoria na nyanda za juu kaskazini mashariki yanayotarajiwa kupata mvua za wastani hadi juu ya wastani, inaweza kuathiri ukuaji wa baadhi ya mazao yasiyohitaji maji mengi, kama vile mahindi, maharagwe na mazao ya mizizi,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles