TMA yatahadharisha mvua kubwa, Dar, Tanga, Zanzibar kuathirika

0
1716

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), imetoa tahadhari ya kunyesha kwa mvua kubwa kati ya kesho Alhamisi Oktoba 17 na Ijumaa katika baadhi ya maeneo nchini.

Kwa mujibu wa mamlaka hiyo maeneo hayo ni ya Ukanda wa Pwani ya Kaskazini kwenye mikoa ya Tanga, Dar es Salaam, Pwani, visiwa vya Unguja na Pemba pamoja na Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro.

“Uwezekano wa mvua kutokea ni wastani na kiwango cha athari zinazoweza kutokea ni baadhi ya makazi kuzungukwa na maji, ucheleweshwaji wa usafiri, kusimama kwa muda kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi na kijamii,” imesema taarifa hiyo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here