32.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 1, 2023

Contact us: [email protected]

TMA yatabiri mvua kubwa mikoa ya Pwani

Na ASHA BANI-DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya hali ya Hewa Tanzania (TMA), imetoa taarifa ya kuanza kunyesha mvua kubwa katika mikoa 11 nchini.

TMA imesema hatua hiyo inatokana na kuanza kwa vipindi  vya mvua kubwa vinavyotarajiwa katika msimu wa Novemba 2018 hadi Aprili mwakani katika mikoa ya Kanda ya Magharibi, Kati na Nyanda za Juu Kusini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TMA, Dk. Agness Kijazi, aliyataja maeneo yatakayoathirika na mvua hizo za juu ya wastani ni Dodoma, Singida, Tabora, Mbeya, Njombe, Iringa, Ruvuma, Kusini mwa Morogoro, Lindi na Mtwara.

Dk.Kijazi alisema utabiri huo ni kwa mikoa inayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka.

“Katika kipindi cha mvua za msimu hali ya unyevunyevu wa udongo kwa ustawi wa mazao na upatikanaji wa chakula cha samaki vinatarajiwa kuimarika katika maeneo mengi.

“Hata hivyo, mazao yasiyohitaji maji mengi kama vile mahindi, maharage na mtama yanaweza kuathiriwa na hali ya unyevunyevu wa kupitiliza na maji kutuama jambo ambalo wakulima inawapasa kuanza kuchukua hatua sasa,” alisema.

Mkurugenzi huyo wa TMA pia aliwatahadharisha wachimbaji wa madini hasa wadogo kuwa makini na ongezeko la maji linaloweza kusababisha mmomonyoko wa ardhi au maji kujaa katika mashimo.

Pia alizishauri mamlaka za miji na majiji kuchukua tahadhari kwa kuhakikisha mifumo ya kupitisha maji inafanya kazi ili kuepusha maji kutuama na kusababisha mafuriko yanayogharimu maisha ya watu na uharibifu wa miundombinu.

“Kutokana na mvua hizi ni vema teknolojia ya uvunaji maji ya mvua iimarishwe ili kukidhi mahitaji ya maji katika kipindi cha baadaye,” alisema Dk. Kijazi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,471FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles