27.3 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

TLS yataka vyuo kufundisha masuala ya mazingira, madini

Na Christina Gauluhanga -Dar-es-salaam

RAIS wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Dk. Rugemeleza Nshala, amesema ipo haja kwa vyuo vikuu hapa nchini kufundisha masuala ya mazingira, madini na mafuta ili kuijengea jamii uelewa wa kulinda rasilimali zilizopo.

Dk. Nshala aliyasema hayo Dar es Salaam mwishoni mwa wiki wakati wa mafunzo ya rasilimali zinazokwisha (SIRD) kwa mawakili wa Serikali, binafsi, wadau wa mazingira na madini kutoka serikalini yaliyofadhiliwa na nchi ya Canada.

Alisema uelewa kuhusu masuala ya madini ni mdogo kwa sababu vyuo vingi hapo awali vilikuwa havifundishi masuala hayo.

“Kwa sasa nchi ina miradi mingi ya uchimbaji mafuta na madini, hivyo ni vyema kuwajengea uwezo wa kielimu wananchi wake ili kuhakikisha taifa linanufaika na rasilimali zake.

“Ni vyema kufanya jitihada za kuwajengea uwezo wa kielimu kuhusu masuala ya madini, mafuta na mazingira wananchi wetu ili waweze kufahamu haki zao,” alisema Nshala.

Kwa upande wake, mshiriki ambaye ni mwanasheria kutoka Baraza la Mazingira (NEMC), Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Naomi Joshua, alisema mabadiliko ya Sheria ya Mazingira ya mwaka 2017 yamechagiza uwezo wa shughuli za kimazingira, hasa katika sekta ya madini tofauti na hapo awali.

Alisema NEMC imekuwa ikijitahidi kufuatilia miradi mbalimbali na kuangalia athari za kimazingira na namna ya utekelezaji kabla ya kuanzisha kwa mradi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles