NYOTA wa muziki nchini Nigeria, Tiwa Savage, amewataka wasanii wa kiume nchini humo kuachana na tabia ya kuomba rushwa ya ngono kwa ajili ya kuwasaidia wasanii wachanga.
Mrembo huyo amedai kwamba kuna baadhi ya wasanii ambao wana tabia ya kutaka kuwasaidia wasanii wa kike ambao ni wachanga kwenye muziki lakini kwa kuwataka watoe rushwa ya ngono ili wawasaidie.
“Kuna wasichana wengi katika tasnia ya muziki kwa sasa na wapo ambao wanatamani kufika hapo ila kuna changamoto kubwa sana hasa pale wanapoomba kufanya kazi na wasanii wa kiume ambao wana majina makubwa.
“Wengi wao wanaombwa kutoa rushwa ya ngono kwa ajili ya kuwasaidia, hivyo wanatakiwa kuwa makini na wasanii hao kwa kuwa wanaweza kuwaharibia mipango ya maisha yao, hata mimi nimepitia huko lakini uwezo wangu ukanifanya niwe hapa nilipo kwa sasa bila misaada yao,” alisema Tiwa.