NYOTA wa muziki nchini Nigeria, Tiwa Savage, amedai kuwa anajuta kuweka wazi mambo yake ya ndoa katika mitandao ya kijamii.
Msanii huyo kwa sasa kazi zake zinasimamiwa na kampuni ya Rock Nation, inayomilikiwa na mkali wa rap nchini Marekani, Jay Z.
Tiwa amedai kuwa kwa siku za hivi karibuni amekuwa akiyaweka mambo yake ya ndoa katika mitandao, hasa baada ya kuhojiwa mara kwa mara, lakini kitendo hicho kimewafanya watu wamzungumzie vibaya.
“Katika kitu ambacho naweza kusema kuwa nimekosea katika maisha yangu ni kuweka wazi mambo yangu ya ndoa, najuta kwa kuwa kuna watu ambao wananiongelea vibaya kutokana na taarifa ambazo niliziongea, kuanzia sasa siwezi kufanya hivyo tena kwa mambo yangu binafsi,” amesema Tiwa