23.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 10, 2024

Contact us: [email protected]

TISTA yajivunia kuongezeka ufaulu elimu ya dini ya Kiislamu

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Tanzania Islamic Studies Teaching Association(TISTA), imetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la saba wa elimu ya dini ya Kiislamu na lugha ya kiarabu, uliofanyika Agosti 14,2024, huku ufaulu na shule zilizofanya mtihani huo zikiongezeka.

Akizungumza na waandishi habari leo Agosti 29, 2024,  jijini Dar es Salaam, Makamu Mwenyekiti wa TISTA,  Shekh Mussa Kundecha amesema jumla ya shule 4,583 kutoka mikoa 28 ya Tanzania Bara na Zanzibar, zilisajiliwa kufanya mtihani huo.

Ameeleza kuwa jumla ya watahiniwa waliosajiliwa kufanya mtihani wa somo la dini ya Kiislamu walikuwa 178,803, wasichana  ni  96,535 sawa na asilimia 54, wakati wavulana ni  82,268 sawa na asilimia 46, huku watahiniwa wenye mahitaji maalu wakiwa saba.

“Kati ya hao watahiniwa waliofanya mtihani ni  163,430 sawa na asilimia  91.4 ya wanafunzi walisajiliwa ambapo wasichana ni 89.887 sawa na asilimia  55 na wavulana ni 73,543 sawa na asilimia 45 na wenye mahitaji maalum walikuwa saba sawa na asilimia 100.Idadi ya watahiniwa ambao hawakufanya mtihani mtihani kutokana na sababu mbalimbali walikuwa 15,373 sawa na asilimia 8.6″

“Idadi ya Halmashauri zilizoshiriki kufanya mtihani huo imeongezeka kutoka 159 mwaka 2023 hadi kufikia  162 mwa 2024 na watahiniwa wameongezeka kutoka  3,975 mwaka 2023 na kufikia 4,583 mwaka 2024”

“Idadi ya watahiniwa waliofaulu kwa kupata madaraja A hadi D ni 153,703  sawa na asilimia 94.1 ya watahiniwa wote 163,430, watahiniwa waliopata daraja E ni 9,727,” amesema Shekh Kundecha.

Kuhusu somo la Lugha ya Kiarabu amesema watahiniwa waliosajili kufanya mtihani huo  walikuwa 10,080, huku walifanikiwa kufanya mtihani ni 1,069.

“Matokeo ya mtihani wa  wa Madrasa, jumla ya watahiniwa waliosajiliwa walikuwa ni  217, waliofanya mtihani 187 sawa na asilimia 86.18. Idadi ya watahiniwa ambao hawakufanya  mtihani kutokana na sababu mbalimbali ni 30 sawa na asilimia 13.82.

“Idadi ya watahiniwa waliofaulu kwa kupata madaraja A hadi D ni 169 sawa na watahiniwa wote 187. Walipata daraja E ni 18 sawa na asilimia 9.6,”  amefafanua Shekh huyo.

 Hata hivyo amewashukuru wadau wote ikiwamo  Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia  kutokana na mafanikio yaliyopatikana.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles