25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 30, 2021

Timu za Kanda ya Ziwa zaanza vibaya Taifa Cup

Derick Milton, Simiyu

Mashindano ya Mpira wa Kikapu Taifa Cup yanayoendelea katika uwanja wa halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu, yanaendelea huku timu kutoka mikoa ya kanda ya ziwa, zikianza vibaya katika michezo yake.

Timu hizo zilizoanza vibaya kwa kufungwa michezo yake ni timu za Simiyu, Mwanza, Mara na Shinyanga. Timu hizo zimeaonekana kuzidiwa mbinu za kimchezo, nguvu kwa wachezaji wake pamoja na kushindwa kuendana na kasi za wachezaji wa timu pinzani.

Katika mchezo wa ufunguzi uliozikutanisha timu kutoka mkoa wa Mara na Singida, Mara walipokea kipigo kwa pointi 74 kwa 67, huku mchezo wa pili, Arusha na Shinyanga, Arusha wakipata pointi 91 kwa 65.

Mchezo wa tatu Mwanza na Dar es Salaam, Mwanza walifungwa kwa pointi 94 kwa 45, huku mchezo wanne ambao ulichezwa majira ya saa kumi, ulizikutanisha wenyeji Simiyu na Tanga, ambapo wenyeji walipokea kipigo cha pointi 100 kwa 54.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,407FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles